Sports

YANGA MABINGWA KOMBE LA ASFC

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam(ASFC) baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati mitatu kwa mmoja dhidi ya Coastal Union

YANGA MABINGWA KOMBE LA ASFC.

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam(ASFC) baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati mitatu kwa mmoja dhidi ya Coastal Union

Fainali hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko mkoani Arusha nchini Tanzania,iliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu zote mbili kumaliza mchezo kwa kutoshana nguvu ya mabao matatu kwa matatu

Coastal union ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la uongozi lililofungwa na mfungaji bora wa michuano hiyo Abdul Suleimani Sopu aliyefunga mabao matatu (hat trick) kwenye fainali ya leo

Mabao ya kusawazisha ya Yanga yalifungwa na kiungo bamia Feisal Salum,Heritier Makambo pamoja na wonder kid Dennis Nkane

Baada ya kunyakuwa ubingwa huo,kwa sasa Yanga imeweka rekodi ya kushinda mataji matatu (treble)katika msimu huu,ambapo mapema mwaka huu waliwafunga mahasimu wao Simba na kunyakua taji la Ngao ya hisani kabla ya kubeba ubingwa wa ligi kuu sambamba na taji la leo la kombe la shirikisho la Azam.

Back to top button