Sports

Kapu la magoli,……..

Emmanuel Dennis

Baada ya mapumziko za Ligi kwa wikiendi iliyopita ili kupisha michezo ya kufuzu kombe la dunia kwa timu za taifa hatimaye michezo ya Ligi kuu imerejea Tena.

Kwa kuanzia na Ligi pendwa na maarufu duniani Ligi kuu nchini Uingereza tumeshuhudia mitanange mbalimbali kwa siku ya jana ya jumamosi. Mchezo wake awali tumeshuhudia Chelsea wakiendelea walipoishia baada ya kuifunga Leicester city mabao matatu kwa bila(3-0) na kuendelea kujikita kileleni. Pia kwa siku ya jana ilikua ni siku nzuri kwa makocha wapya Dean Smith wa Norwich pamoja na Steven Gerrard wa Astonvilla baada ya kuanza na ushindi katika vilabu vyao. Norwich walipata ushindi wao wa Kwanza kwenye Ligi msimu huu kwa kuifunga Southampton mabao 2-1. Pia Astonvilla baada ya kutopata ushindi kwa mechi zaidi ya tano kwenye Ligi Jana ilipata ushindi wa mabao Mawili kwa bila dhidi ya Brighton.

Liverpool ikashinda mabao manne kwa bila dhidi ya Washika bunduki wa London timu ya Arsenal. Arsenal walicheza michezo minane ya Ligi kuu bila kufungwa hivyo Liverpool wakafanikiwa kusitisha mbio hizo za Arsenal. Arsenal wanaendelea kusalia katika nafasi ya tano huku Liverpool wakipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo.

Kabla sijatia nukta , mechi iliyoishika hisia kubwa kwa siku ya Jana ilikua mechi ya Watford dhidi ya Manchester United. Ilikua mechi ya kufa au kupona kwa vijana wa Ole Gunnar. Baada ya dakika 90 kuisha habari ikabaki ileile Manchester United kufungwa mabao 4-1 huku kapteni wao Harry Maguire akipewa kadi nyekundu. Ushindi huo wa Watford umekua msumari wa mwisho kwa Ole Gunnar ndani ya viunga vya Old Trafford.

             

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker