Sports

MASAIBU YA NICK MWENDWA

PICHA|Hisani.

Rais wa Shirikisho la Soka Nchini,FKF,Nick Mwendwa anaendelea kukumbwa na Msururu wa masaibu yanayomuandama.Leo hii imeripotiwa kuwa Mwendwa ameweza kukamatwa na maafisa wa polisi.Tukio hili linatokea siku moja tu baada ya Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohammed kubuni Kamati itakayoangazia Masuala ya Kandanda Nchini kwa muda wa miezi Sita.

Tukio hili limefanyika pindi tu baada ya Nick Mwendwa Kukutana na wachezaji wa Timu ya Soka ya Taifa Harambee Stars.

Siku ya Alhamisi,Wizara ya Michezo iliweza kumteua Jaji Mstaafu Aaron Ringeria Kama mwenyekiti wa Kamati iliyobuniwa.Walioteuliwa pia Ni pamoja na Joseph Masiga,Kocha wa Klabu ya Kenya Police FC John ‘Bobby’ Ogola,Fatuma Adan,Philip Musyimi, Anthony Isayi,Elisha Kiplagat,Hassan Haji, Fredrick Tureisa,Mwangi Muthee,Neddy Atieno,Ali Amour,Titus Kasuve,Moses Oyugi pamoja na Richard Omwela.

Kamati hii iliyobuniwa imeweza kusitisha shughuli zote za Kandanda Nchini kuanzia kwa Ligi ya Division 1, National Super League pamoja na Ligi kuu Nchini, FKF Premier League.

             

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker