PoliticsTrending

WAKENYA HAWAKO SALAMA MIKONONI MWA WILLIAM RUTO

Picha/Hisani

WAKENYA HAWAKO SALAMA MIKONONI MWA WILLIAM RUTO

Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria kwa mara nyingine tena amemrushia vijembe Naibu Rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini, Jumapili, Novemba 7, Kuria alionyesha wasiwasi yake na uongozi wa Ruto akidai kuwa taifa halitakuwa katika mikono salama na utawala wake. Pia aliongeza kuwa utawala wa Ruto utakuwa wa ‘udikteta’ ambao utakuwa ukitumia nguvu zaidi kinyume na katiba ambapo ni tatizo kubwa linalokumba Kenya. Read Kuria pia hakumsaza kinara wa ODM Raila Odinga katika mashambulizi yake akisema kuwa wagombea wote wa urais ni wabaya zaidi. Read also Cate Waru Mwanasiasa huyo mashuhuri pia aliongezea kuwa wagombea wote wa urais ni hatari kwa taifa na wanahitaji mtu wa kupunguza ubaya huo kupitia kwa kumchagua mgombea mwenza tofauti.Alipoulizwa mtazamo wake kuhusu kiongozi wa Narc Kenya, Martha Karua, ambaye alimpendekeza kuwa naibu wa rais, Kuria alifichua kuwa ana utata naye. Huku akikataliwa na Kuria, kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga amepigwa jeki kisiasa katika azma yake ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu 2022 ili kumrithi Rais Uhuru Kenyatta, baada ya wabunge wa Nairobi kutangaza watamuunga mkono. Kulingana na wanasiasa hao, Raila aliungwa mkono na jamii zote zilizoishi jijini, na pia kupata uungwaji mkono na wenyeji wa maeneo ya Mt Kenya. Wanyonyi na Aladwa walisema hapana shaka Raila atapigiwa kura na Waluhya kwa wingi kwa kuwa ni mojawapo ya jamii zilizo na idaid kubwa ya wapiga kura jijini Nairobi. Wabunge hao ni pamoja na Tim Wanyonyi, George Aladwa, Godfrey Osotsi na Muriithi Mwenje, waliosema hakuna kitakachoweza kumzuia Raila kutwaa urais mwaka ujao.

Related Articles

Back to top button