World

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera kuwasili Kenya kwa ziara ya Serikali ya siku tatu

Lazarus Chakwera

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera kuwasili Kenya kwa ziara ya Serikali ya siku tatu

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera anatarajiwa kuwasili Kenya Jumanne, Oktoba 19 kwa ziara ya Serikali ya siku tatu.

Bwana Chakwera, ambaye ataandamana na Mke wake Monica Chakwera, atakuwa Mgeni Mkuu katika sherehe za Siku ya Mashujaa ya mwaka huu ambayo itafanyika katika uwanja wa Wang’uru katika Kaunti ya Kirinyaga Jumatano.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, msemaji wa Ikulu Kanze Dena alisema Rais wa Malawi na wajumbe wake watapokelewa rasmi Ikulu, Nairobi na Rais Uhuru Kenyatta Alhamisi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button

Adblock Detected

turnoff Ad blocker to view the site